...

Open login
Mlipuko wa guruneti, nchini Thai, wajeruhi mmoja.
Written by Mwakoyo Vicky    Friday, 30 July 2010 07:13    PDF Print E-mail

Utawala bungeni, nchini Uganda umetangaza vikwazo vipya ili kupunguza kukosa kuhudhuria kwa wabunge, bungeni. Spika Edward Ssekandi alisema kuwa kuanzia mwaka huu wa fedha, mbunge yeyote atakayekosa kuhudhuria bunge bila ya kuomba ruhusa atasimamishwa.

 

Kwengineko Afrika, wakati habari za rushwa zikiendelea kutawala harakati za kuwania ubunge kwa tiketi ya CCM, kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Kilimanjaro, nchini Tanzania, Alexander Budigila amehamishwa na kushushwa cheo siku chache baada ya maofisa wake kumkamata mkuu wa wilaya ya Kasulu, Betty Machangu. Huku harakati za kuwania ubunge kwa tiketi ya CCM zikielekea ukingoni, mbunge wa jimbo la Arusha ambaye anamaliza muda wake, Felix Mrema juzi alinaswa na Takukuru kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya rushwa, huku kukiwa na habari ambazo Takukuru inasita kuziweka bayana za kigogo mmoja wa CCM kukamatwa kwa tuhuma hizo mkoani Morogoro.

 

Wafanyakazi wa uokoaji wanawatafuta manusura wa ajali ya boti katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambapo watu 140 wanahofiwa kufariki baada ya boti hiyo iliyobeba abiria kuzidi uwezo wake na kupinduka katika mto. Boti hiyo iliyokuwa na wafanyakazi na abiria wapatao mia mbili inaaminika kugonga kingo za mchanga au mwamba, Jumatano katika maunganiko ya mto Congo, katika jimbo la Bandundu liliopo magharibi mwa nchi hiyo; watu themanini wametangazwa kufariki.

 

Katika habari za kimataifa, rais wa Syria Bashar al-Assad na mfalme Abdullah wa Saudi Arabia wanatarajiwa kutembelea Lebanon. Ni ziara ya kwanza ya Bw assad kwenda nchini humo tangu mwaka 2005, ambapo Syria ililazimika kutoa vikosi vyake baada ya kuuliwa kwa waziri mkuu Rafik Hariri.

Guruneti limelipuka jijini Bangkok, Thailand, na kujeruhi mwanamume mmoja vibaya sana, polisi wamesema. Imetokea baada ya mlipuko siku tano zilizopita na maandamano yanayopinga serikali mwezi wa Aprili na Mei.

Ili kupata habari zaidi za kimataifa, tuma neno KIMATAIFA kwa 8198.

 

 

 

Last Updated ( Friday, 30 July 2010 07:30 )