...

Open login
Wapiganaji wa Kisomali wasitisha maasi Ethiopia
Written by Mwakoyo Vicky    Thursday, 29 July 2010 06:59    PDF Print E-mail

 

Mshahara wa mkurugenzi mkuu aliyesimamishwa wa National Forestry Authority, nchini Uganda, Bw Damian Akankwasa ulitosha kufikisha sh100m kama fungu la sh900m zilizodaiwa kuibiwa na mke wake, mahakama ilisikia. “Nilikuwa nalipwa sh10m na baada ya kupandishwa cheo mshahara wangu uliongezwa hadi sh11m,” alisema haya alipokuwa anahojiwa; pia alisema alikuwa katibu wa bodi la NFA na alilipwa shilingi laki 2 kila kikao pamoja na nyongeza ya sh2.53m.

 

Kwengineko, serikali ya Ethiopia leo inatarajiwa kusaini mkataba wa maridhiano kati yake na kundi la waasi la United Western Somali Liberation Front. Kundi la UWSLF mwezi April mwaka huu lilikubali kuweka chini silaha zao baada ya mazungumzo ya siri kati yake na serikali ya mjini Addis Ababa. Kukubali kwa muafaka na serikali, kundi hilo linamaliza miongo miwili ya harakati za kijeshi dhidi ya serikali , wakati huo likiwa na nia ya kujitenga na Ethiopia.

 

Mamlaka nchini Nigeria zinasema zitafikisha mashirika, taasisi na watu binafsi wapatao 260, katika mahakama maalum kuhusiana na shughuli zinazokwenda kinyume cha sheria katika soko la hisa la nchi hiyo. Washukiwa hao hawajatajwa bado, lakini ni pamoja na madalali wa hisa, wahasibu na wanasheria. Wanashukiwa kwa kufanya uhalifu wa kifedha kama vile kupanga bei za vitu, kupanga hila za kubadili bei za hisa, udanganyifu na kufanya biashara ndani kwa ndani.

 

Jaji wa mahakama moja katika jimbo la Arizona nchini Marekani, amezuia kutekelezwa kwa vipengele tata vya sheria kuhusiana na uhamiaji ambavyo vilitarajiwa kuanza kutekelezwa leo. Serikali kuu ya Marekani na makundi ya kutetea haki za binadamu wamepinga sheria hiyo ya uhamiaji ambayo ingesababisha watu kuchunguzwa zaidi.

Ili kupata habari zaidi za Afrika Mashariki, tuma neno E.AFRIKA kwa 8198

 

 

 

 

Last Updated ( Thursday, 29 July 2010 07:02 )