| Hali ya usalama Darfur yazidi kuzorota | ||||
|
|
Muungano wa Afrika (AU), utasaidia vikosi vinavyoleta amani nchini Somalia ila hawatawakubalia kushambulia waasi wa kiislamu, ijapokuwa wamehimizwa na nchi kadhaa baada ya waasi hao kuua watu 76 katika mashambulio ya mabomu nchini Uganda. Wanadiplomasia wa Afrika katika mkutano wa muungano wa Afrika (AU) walisema kuwa uwezekano wa kukubalia vikosi hivyo kushambulia waasi hao unaweza kukataliwa ila kifungu cha 8,100 kuhusu idadi ya vikosi kinachojulikana kama AMISOM kitapandishwa. Kwengineko Afrika, ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa inasema kwamba machafuko yaliongezeka huko Darfur mara tu baada ya kufanyika kwa uchaguzi wa kitaifa mwezi wa Aprili mwaka huu huko Sudan. Katibu Mkuu huyo Ban Ki Moon amesema, katika mwezi wa Mei pekee, zaidi ya watu 400 waliuawa katika mapigano kati ya vikundi vya waasi na majeshi huko Darfur. Mmoja wa wabunge wa bunge la Zimbabwe, Roy Bennett, ambaye ni mzungu ameiambia BBC kuwa anaamini kwa sasa Zimbabwe inaendeshwa na utawala wa kijeshi. Bwana Bennett, ambaye ni mshirika wa karibu wa waziri mkuu, Morgan Tsvangirai, amesema anaamini Rais Mugabe analazimishwa na jeshi kuendelea kutawala nchi hiyo. Bwana Bennett, ambaye ni mkulima wa zamani, amezuiliwa kuchukua wadhifa wa unaibu waziri wa kilimo katika serikali ya umoja wa kitaifa kutokana na taratibu za kisheria zinazorudiwa rudiwa. Kwenya habari za kimataifa, mkaguzi mkuu wa silaha wa Umoja wa Mataifa, kabla ya mgogoro wa Iraq, Hans Blix, amesema Uingereza iliingia katika vita vya kuishambulia Iraq ambavyo havikuwa na sababu kisheria. Bwana Blix alikuwa akizungumza na BBC mjini London, baada ya kutoa ushahidi wake mbele ya tume inayosikiliza sababu za kuivamia Iraq kijeshi. Katika habari za michezo, shirikisho la soka la Argentina limemtimua mchezaji wao mashuhuri wa zamani Diego Maradona kama kocha wa timu ya taifa. Inaripotiwa kuwa Diego Maradona au alivyotambuliwa kufuatia kombe la dunia la mwaka 1986 ''mkono wa mungu'', alitimuliwa baada ya kukataa masharti aliyopewa ili aongezewa mkataba. Mojawapo ya masharti hayo, ni kuwashirikisha wasaidizi wenye utalaam wa soka , jambo alilolikataa. Ili kupata habari zaid za kimataifa, tuma neno KIMATAIFA kwa 8198 |
| Last Updated ( Wednesday, 28 July 2010 09:17 ) |


